Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Uwezo: Uongozi wa WanafunziMfano

Capacity: Student Leadership

SIKU 5 YA 5

1 Timotheo 4:12-16
Inaweza kuwa rahisi kuamini uongo kuwa wewe ni mdogo sana kufanya mambo makubwa. Lakini hiyo si ukweli. Wewe, sasa hivi leo, unauwezo wa kuweka mfano kwa KILA MTU
maishani mwako. Unaweza leta mabadiliko, na hauhitaji kungoja hadi uwe mkubwa au mzee au mwenye hekima zaidi au mwenye kukomaa zaidi. Mungu atakutumia jinsi ulivyo sasa. Kwa hivyo, ishi kwa kile Mungu amekuita ufanye na kile amekuumba uwe. Jisalimishe kwa hayo mambo kabisa. Ukifanya, utaona Mungu akifanya maajabu, mambo ya kusisimua katika na kupitia
maisha yako. Nenda na uishi maisha ukifurahia Mungu, kile ambacho amekuumba uwe. Mtukuze kwa chote ulicho nacho na kwa nafsi yako yote.
siku 4

Kuhusu Mpango huu

Capacity: Student Leadership

Mungu anakuitia Mambo Makubwa. Sio tu ukishakuwa mkubwa bali sasa hivi. Mpango huu utakutia moyo na kukuonyesha jinsi ya kuongezeka na muongozo wa unapostahili kuwa maishani sasa hivi. Mungu anaweza na atakutumia kwa njia za ajabu. Swali ni—utamkubalia?

More

We would like to thank Switch, a ministry LifeChurch.tv, for providing this plan. For more information, please visit: www.lifechurch.tv