Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Mkazo wa mtume Paulo katika somo la leo ni kuonyesha kwamba ujumbe wake watoka moja kwa moja kwa Mungu. Angalia kwa mfano anavyosema katika m.12, Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo. Maana yake si kwamba sisi wa leo tujitenge na Wakristo wengine ili kupata ufunuo maalum. Bali hata mtume Paulo baada ya muda mrefu alipanda kwenda Yerusalemu ili kuwaona viongozi hapo. Kefa ni sawa na mtume Petro. Paulo anaeleza kwa kusema, Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu (m.15-16). Hii inaonyesha kwamba kumpokea Kristo ni neema kutoka kwa Mungu. Vilevile utume alio nao, Paulo anaona ameupata kwa neema.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/