Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Kumwamini Mungu katika MatesoMfano

BibleProject | Kumwamini Mungu katika Mateso

SIKU 3 YA 6

Ayubu alipoteza kila kitu—mali yake, watoto wake, na afya yake. Lakini hata hivyo, kinyume na alivyotarajia mshtaki, Ayubu anakataa kumlaani Mungu. Hata hivyo, anailaani siku ambayo alizaliwa. Maumivu yake ni makali sana kwamba anatamani hangezaliwa. Je, Mungu anamjibu vipi Ayubu?

Jibu la Mungu linakuja mwishoni mwa kitabu, na ni kinyume na maneno ya Ayubu kuhusu kuzaliwa kwake. Ayubu anasema, "hebu iwe giza," lakini Mungu anakumbuka jinsi alivyoumba nuru na kuzuia giza. Mungu anaonyesha kwamba yeye ndiye huzuia uovu na machafuko, na huruhusu nuru kushinda. Ayubu anajuta kuzaliwa, lakini Mungu anajionyesha kuwa muumbaji wa ulimwengu. Mungu anajali alichoumba kama baba mwenye busara na mama mwenye uchungu wa uzazi. Yuko tayari kuteseka ili uumbaji ustawi.

Hivyo tunapoangalia mateso ya ayubu, Mungu anataka tufahamu kwamba Yuko nasi. Mungu anajua uchungu wetu. Anahisi tunachohisi. Inamgharimu kwa maumivu makali kutoa uzima na kuzuia giza ulimwenguni. Unapoteseka bila kustahili na mateso yanapokusonga hadi unapoteza matumaini, amini kuwa Mungu yupo kazini akidhibiti majanga na kutoa uhai.

Tafakari:
1) Je, ni mateso gani unayoyaona ulimwenguni au katika maisha yako?
2) Je, Mungu anafanya kazi vipi kutoa uhai na kupanga mambo katika hali hiyo ya uchungu?
3) Je, ni vipi ambavyo Yesu aliteseka ili kuzuia machafuko na kuleta uhai?

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Kumwamini Mungu katika Mateso

Je, tunawezaje kumwamini Mungu hata pale tunapoteseka bila kustahili? Jiunge nasi katika muongozo huu wa wa siku zita unaotazama simulizi ya Ayubu na ufahamu jinsi kuamini hekima ya Mungu kunaonekaje hata katika vipindi tunapokumbana na magumu.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili