BibleProject | Kumwamini Mungu katika MatesoMfano
Kitabu cha Ayubu kinamalizikia Mungu akirejesha kila kitu ambacho Ayubu alipoteza. Hii inatufundisha nini? Kwanza, hebu tukumbuke kwamba simulizi hii tayari imetuonyesha kwamba haki ya Mungu ni kuu kuliko mtazamo kuwa wenye haki hutunzwa nao waovu huadhibiwa. Japo ni kweli kwamba Mungu huwazawadia wanaomcha (Waebrania 11:6) na kuwa huadhibu uovu kwa haki (Isaya 13:11), sifa hizi za Mungu hazifanyi kazi kila wakati katika njia ambazo tunatarajia. Hivyo Mungu kurejesha afya na mali ya Ayubu haikuwa kwa sababu ya utakatifu wa Ayubu, na pia Ayubu kupoteza mali yake haikuwa adhabu kutoka kwa Mungu. Hitimisho la kitabu linaonyesha kuwa haijalishi yanayotendeka maishani mwetu, mema au mabaya, tunaweza kumtegemea Mungu kuwa mkarimu na tunaweza kutegemea nguvu zake za kurejesha.
Tunapomalizia siku ya mwisho kwenye mwongozo wa kusoma, hebu tupitie tulichojifunza. Tazama video yetu ya Muhtasari kuhusu kitabu cha Ayubu ili uangalie mpangilio wake na mtiririko wa matukio.
TAFAKARI:
1) Je, unaweza kuandaa muhtasari wako mwenyewe kuhusu ujumbe wa video uliyotazama?
2) Je, mwongozo huu wa kusoma umekusaidia vipi kuelewa au kuchambua kitabu cha Ayubu?
3)Je, unaweza kushiriki mwongozo huu na nani siku ya leo?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Je, tunawezaje kumwamini Mungu hata pale tunapoteseka bila kustahili? Jiunge nasi katika muongozo huu wa wa siku zita unaotazama simulizi ya Ayubu na ufahamu jinsi kuamini hekima ya Mungu kunaonekaje hata katika vipindi tunapokumbana na magumu.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili