Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022

SIKU 6 YA 31

Katika maisha twakutana na dhiki nyingi. Kupungukiwa na kushindwa kupata mahitaji na matakwa yetu ni chanzo cha dhiki nyingi. Kudhulumiwa na wasio haki pia husumbua watu, hivyo kuwa chanzo cha taabu. La maana si orodha ndefu ya dhiki na vyanzo vyake bali ni uhakika wa msaada. Je, lipo tumaini la msaada kwa walio katika dhiki? Daudi awezaje kusema,Sasa najua kuwa Bwana aniokoa?(m.6) Rudia m.1, 5 na 7 ukizingatia maana ya kulifahamuJinala Bwana.Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue, ... Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote, ... Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. Liitie Jina hilo na kumtegemea Yeye siku zote.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/