Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022

SIKU 5 YA 31

Adhabu inapotekelezwa, wengine wanatoa malalamiko tu juu ya maumivu wanayopata, na kudhihaki (m.14,Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote). Lakini Yeremia, mtunzi waMaombolezo, anajihusisha na watu wake wanaoteseka. Maumivu yao ni ya kwake. Tena anatambua kuwa mateso hayo ni hukumu ya Mungu iliyo ya haki. Rudia m.13 uone jinsi Yeremia anavyoeleza kwa hisia kuhusu mateso yaliyompata: Bwanaamenichoma viuno Kwa mishale ya podo lake. Yeremia ametumia mifano mingi kufananisha ukali wa mateso hayo. Mungu anaposema atakuja kuhukumu, ni jambo la kweli kabisa. Yatupasa kuogopa, kisha tutubu ili tusiingie katika mateso makali zaidi, kama yale anayotaja Yesu katika Mt 25:30:Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/