Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 11 YA 31

Mara ya tatu Isaka alipochimba kisima katika bonde la Gerari, Wafilisti hawakuja tena kukigombania (m.22, Isaka akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania). Alikuwa na uwezo wa kuwashinda wale Wafilisti kwa nguvu (m.16, Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi). Lakini ni mpole, hakupenda vita. Aliamua kumtegemea Bwana tu! Kwa hiyo alipofanikiwa, mara moja akampa Bwana utukufu, akisema, Sasa Bwana ametufanyia nafasi (m.22)! Kutokana na jambo hili na baraka nyingine nyingi, Isaka akaamua kwenda kumwabudu Mungu kipekee Beer-sheba (rudia m.23-25 ukipenda). Pia Ibrahimu aliabudu hapo (21:33, Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la Bwana Mungu wa milele).

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/