Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Kwao waliotegemea Babeli, kuanguka kwake kutakuwa hasara kubwa, lakini kwa watakatifu, mitume na manabii unatolewa mwito wa kufurahi. Maana sasa Mungu ameuhukumu utawala wa mpinga Kristo uliosimamia kuwaua. Kama jiwe litupwavyo baharini hautainuka tena, na waumini wamepewa haki yao (m.20, Furahini juu yake, enyi mbingu, nanyi watakatifu na mitume na manabii; kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake). Hakika Bwana Mungu hudhibiti mambo yote duniani. Atazikomesha taasisi na taratibu za maisha za kishetani. Ni heri kwako na kwangu ikiwa kujua haya kunaleta furaha na nguvu mpya kumtegemea Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/