Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

SIKU 14 YA 31

Shetani atafanya hima akitumia nafasi ya muda mchache alioachiwa na Mungu, ili kuwadanganya mataifa. Atakusanya jeshi kubwa dhidi ya watakatifu katika ”mji uliopendwa” (= Yerusalemu). Watakatifu hawana nguvu kama maadui zao. Wakizingirwa hivyo, je, wana msaada wowote? Kumbuka, wokovu na utukufu na nguvu zina Bwana Mungu wetu (Ufu 19:1-2). Atashusha moto kuwala maadui (m.9 ambapo imeandikwa moto huu ukashuka kutoka mbinguni), na atamhukumu shetani, mkuu wao, adhabu ya milele pamoja na yule mnyama na nabii wa uongo katika ziwa la moto.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/