Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

SIKU 6 YA 31

Mpinga Kristo na walioungana na utawala wake wataonekana kana kwamba wana umoja na nguvu nyingi, lakini watashindwa na Bwana Yesu. Maana ni Mungu aliyewatia nia moja ili waangamize utawala wao wenyewe na kutimiza neno la hukumu ya Mungu. Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maeno ya Mungu yatimizwe (m.17). Ndivyo Bwana Yesu atavyowashinda maadui zake na kuyadhibiti matukio yote katika historia ya dunia. Usipoteze neema ya kujua haya; mwamini Kristo Yesu, Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme, ili uwe upande wa washindi waitwao wateule na waaminifu (m.14, Walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu).

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/