Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Dhambi, uasi na kutomcha Mungu huleta matukio ya kutisha. Kama ingekuwa tu misukosuko ya kawaida ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, mwanasiasa hodari au mchumi bora au mwanasayansi mkuu angeweza kuleta unafuu. Lakini yatakapotokea maafa ya asili ya namna hii tuliyosoma, hakuna awezaye! Ni nguvu za mbinguni zinazotikisika. Imeoneshwa katika m.17, 19 na 21 kwa kutaja “anga”, “kikombe cha mvinyo ya dhadhabu ya hasira yake” Mungu, na “mvua ya mawe”. Ni hukumu kubwa ya Mungu na ya mwisho juu ya utawala wa mpinga Kristo. Ni heri haya yakitukumbusha ukuu wa Mungu, tupate kumcha Yeye badala ya kumtukana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/