Upendo Wa BureMfano
Kutoka Maisha ya changamoto na shida hadi Maisha ya Unyonge
Watu wanaolisha au kuwachunga nguruwe wanaanza kuiga tabia za nguruwe. Njaa iliyomkumba Mwana Mpotevu ilimlazimisha kula chakula kibofu sana lakini, hakunawiri au kushibishwa na chakula hiki. Alianza maisha yake akiwa anafuata anasa, mafanikio, mapenzi na raha lakini alipata vitalu au vizuizi kote alikoenda. Baada ya kutapanya mali yake yote, alijipata kuwa mnyonge na bado, hakutosheka katika maisha yake.
Mithali 15:21 inatueleza hivi, “Upumbavu ni furaha kwake aliyepungukiwa na akili; Bali mwenye ufahamu huunyosha mwenendo wake.” Upungufu wa Mwana Mpotevu ulisababisha raha za wakati mfupi, lakini, alihitaji ujuzi mufti na ukosefu wa ujuzi huu ulimwacha katika shida kubwa, shida ambazo hakutegemea kupata. Ninakutana na watu wengi sana walio katika vyumba au makao ya nguruwe, watu ‘wanaokula’ vyakula vibofu kabisa wakijaribu kutosheleza upweke ulio katika mioyo yao. Ilhali, haijalishi jinsi wanavyojaribu, bado wanabakia wakiwa wapweke, katika hali ya kutoridhika na mioyo yenye machungu kama shimo la giza - roho tupu zinazohitaji kujazwa….na hakuna anayeweza kuwapa riziki inayoleta mabadilko.
Watu wengi wanacheza karata ya kadi katika maisha yao, matokeo yakiwa mahusiano, mafanikio ya kifedha, umaarufu katika jumuiya au kuheshimika au kupata mamlaka katika mambo ya kidini na kuzoroteka hadi kujiunga na tabia za ngono, kutumia madawa za kulevya na burudani zisiofaa. Haijalishi wanapojipata maishani, yaani, wakiwa upande wa hekima au maisha ya uharibifu, inakuwa wazi kwamba roho unaoishi milele hauwezi kunusurishwa na mambo ya kidunia. Basi, safari ya Mwana Mpotevu likuwa ya mviringo katika mauti iliyo vigumu sana kuepuka mpaka wakati alirudisha fahamu na kuwaza, “Mambo haya yalifanyika vipi? Nilifikia hapa vipi? Kunaye atakaye nisaidia? Au, nitateketea katika changamoto zangu?”
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kunayo kusudi au sababu la maana sana katika maisha yako inayopita fikira au mawazo yako. Unaifahamu. Unahisi jambo hili moyoni mwako. Kijitabu hiki kitakuwa nguzo ya kubadilisha maisha ya wote watakayo kisoma. Funzo au hadithi ya Mwana Mpotevu imegusa mioyo ya mamillioni kote duniani. Siku saba zijayo, utapata kufahamu funzo hili kwa mfano tofauti.
More
Tungependa kumshukuru CfaN Christ Kwa Mataifa Yote kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://cfan.org/?office=za&language=en