Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Upendo Wa BureMfano

Upendo Wa Bure

SIKU 2 YA 5

Kutoka Upendo wa Bure hadi Maisha Hovyo

Kijana aliyekuwa anelekea kuwa Mwana Mpotevu, ambaye alikuwa mdogo wa ndugu wawili, alitenda jambo la kuhuzunisha sana, jambo la kumkosea heshima Baba yake na kudharau mapenzi ya dhati au ya bure Baba yake alimpa mwanawe. Kwa ufupi, alimwambia Baba yake”Ninajua bado ungali hai, lakini, siwezi kungoja tena - ninataka urithi wangu sasa.” Baba yake hakuwa na jukumu la kugawa mali yake lakini, kwa kitendo cha kushangaza, alikubali ombi la mwanawe na kugawa mali yake vilivyo, kisha akampa mwanawe mdogo urithi wake.

Kwa muda usiokuwa mrefu, Kijana huyu alichukuwa hela zake zote na kujishughulisha na maisha ya hali ya juu. Aliishi maisha ya anasa, katika Jiji kuu. Ingawa Bibilia haifafanui kikamilifu shughuli zake huko mjini, tunapata kujua kwamba “akakusanya vitu vyote alivyokuwa navyo akaenda nchi ya mbali akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa.” (Luka 15:13) Inamaanisha kwamba alikuwa anaishi maisha hovyo - bila fikra za kesho, bila kujali kamwe ila kufuata msisimko alioupata katika nyakati fupi au chache za raha. Hakuwajli familia/jamii yake. Hakujalishwa na afya yake, kazi yake, sifa zake au mfano aliotoa kwa jumuiya yake - yote yalikuwa duni. Aliishi kupata msisimko wa raha za kimwili. 

Mtazamo huu wa maisha unaoenezwa katika matelevisheni na filamu ni jinsi watu wengi wanvyoishi maisha yao - lakini, mtindo huu ni wa ubinafsi mkuu na kutojibika. Tabia hii hailengi mbali kwenye fikira za mtu, ni tabia za mtu ambaye hajakomaa na ni tabia haribifu sana inayoelekeza mtu katika njia alioypitia Mwana Mpotevu na kukosa kabisa lengo la maisha. Maisha haya ya hovyo yanatilia maanani raha na starehe na msisimko wa wakati mfupi tu, kuliko mambo yote mengine yenye msingi bora. Niamini kwa kweli, ingawa Mwana Mpotevu alikuwa anapiga debe la maisha ya uharibifu, alipata kujuta.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Upendo Wa Bure

Kunayo kusudi au sababu la maana sana katika maisha yako inayopita fikira au mawazo yako. Unaifahamu. Unahisi jambo hili moyoni mwako. Kijitabu hiki kitakuwa nguzo ya kubadilisha maisha ya wote watakayo kisoma. Funzo au hadithi ya Mwana Mpotevu imegusa mioyo ya mamillioni kote duniani. Siku saba zijayo, utapata kufahamu funzo hili kwa mfano tofauti.

More

Tungependa kumshukuru CfaN Christ Kwa Mataifa Yote kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://cfan.org/?office=za&language=en