Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Upendo Wa BureMfano

Upendo Wa Bure

SIKU 3 YA 5

Kutoka Kuishi Hovyo hadi Maisha Duni

Mali au urithi aliopata kutoka Baba yake ilizoroteka kwa haraka na kusababisha bahati mbaya iliyomletea uharibifu kamili ya kifedha. Wakati pesa zaske zilipoisha kabisa, marafiki wake pia walitoweka. Isitoshe, janga kuu likaanza akawa yuko mpweke kabisa! Watu wengi walikuwa na njaa ikawa hakuna angeweza kumsaidia - hangeweza hata kujisaidia mwenyewe.

Luka 15:14-16 inaeleza jinsi alivyongangana kupata riziki. “Baada ya kutumia kila kitu alichokuwa nacho, kukawa na njaa kali katika nchi ile yote naye akawa hana cho chote. 15 Kwa hiyo akaomba kibarua kwa raia mmoja wa nchi hiyo aliyemtuma shambani kwake kulisha nguruwe. 16 Akatamani kujishibisha kwa maganda waliyokuwa wanakula nguruwe, wala hakuna mtu aliyempa cho chote cha kula.”

Mstari wa 14 unasema kwamba alikuwa “katika shida.” Tazama kwa muda, mitindo yake ya ubinafsi yalimwacha Mwana Mpotevu bila uwezo wa kupata usaidizi. Alikuwa hana chochote na mwenye shida. Kinachoshangaza kweli ni jinsi alivyotapanya pesa zake zote akijivinjari na kwa matumizi ya kimwili badala ya kutosheka na kuhifadhi urithi wake, alibaki akiwa mpweke kuliko mbeleni. Kilele cha shida zake kilikuwa wakati aliajiriwa kufanya kazi ya chini kabisa - kulisha nguruwe na kuishi nao.

Haya ni matokeo ya hakika “kuishi maisha ya hovyo na anasa” na mwelekezo wa kweli katika maisha haya duni. Furaha inadumu kwa muda, wakati njaa za maisha zinapotokea, unakuwa mtu mwenye masikitiko, mwenye kinyongo na kisasi, ambaye hana faida kwako binafsi au kwa mtu mwingine yeyote. Badala ya kuwa mtu anayejihusisha na kazi ya punguza shida na changamoto duniani, unakuwa mojawapo wa changamoto zilizoko.

Basi, alikuwa pale, akiishi na nguruwe na mtazamo au fikra za kujilaumu kuhusu safari yake kutoka maisha upendo wa dhati hadi maisha ya anasa mpaka maisha ya unyonge.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Upendo Wa Bure

Kunayo kusudi au sababu la maana sana katika maisha yako inayopita fikira au mawazo yako. Unaifahamu. Unahisi jambo hili moyoni mwako. Kijitabu hiki kitakuwa nguzo ya kubadilisha maisha ya wote watakayo kisoma. Funzo au hadithi ya Mwana Mpotevu imegusa mioyo ya mamillioni kote duniani. Siku saba zijayo, utapata kufahamu funzo hili kwa mfano tofauti.

More

Tungependa kumshukuru CfaN Christ Kwa Mataifa Yote kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://cfan.org/?office=za&language=en