Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano
Yesu alipoanza kazi yake rasmi, alitoka Nazareti na kuhamia Kapernaumu. Kwa hiyo imeandikwa katika m.1 kwamba yumo nyumbani. Sababu ya Yesu kuhamia huko imeelezwa ifuatavyo katika Mt 4:12-16: Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia. Sehemu hiyo ya nchi iliitwa Galilaya. Wayahudi wa sehemu ya Yerusalemu na Uyahudi hawakujali Wayahudi waliokaa Galilaya. Hata hivyo Yesu aliamua kufanya kazi sana katika sehemu hii ya nchi kuliko sehemu nyingine. Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya (1:39)! Kuondoa dhambi kulikuwa ni shabaha kuu ya Yesu (m.5, Yesu alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako). Maana uzima wa milele ni muhimu kuliko uzima wa maisha haya. Basi, zingatia swali la Yesu katika Mk 8:36-38: Itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake? Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz