Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 2 YA 40

Mariamu alipokaribia kujifungua, yeye na mchumba wake, Yusufu, wanahitaji kwenda mji wa Bethlehemu kujiandikisha kwa sensa iliyoamuriwa na Kaisari Augusto. Wanafika, na Mariamu anapatwa na uchungu wa kuzaa. Hawawezi kupata chumba cha wageni na sehemu pekee iliyopo ni zizi la wanyama. Mariamu anajifungua na kumweka mwana atakayekuwa mfalme wa Israeli horini.

Karibu na alipozaliwa mwana, wachungaji wako makondeni wakilisha mifugo yao kisha ghafla malaika mwenye utukufu anawatokea. Tukio hili, bila shaka, linawatisha. Lakini malaika anawaeleza wafurahie kwa sababu Mwokozi amezaliwa. Wanaelezwa kuwa watampata mtoto amevikwa nguo na amelazwa horini. Malaika wengi wanatokea ili kusherehekea kwa kumsifu Mungu aliyeleta amani yake ulimwenguni. Wachungaji wanaondoka haraka kwenda kumtafuta mtoto. Wanampata mtoto Yesu horini kama alivyosema malaika. Wanastaajabu. Wanaeneza habari za walioyashuhudia na kila anayesikia habari hizi anashangaa.

Hakuna aliyetarajia kuwa Mungu angejitokeza namna hii––kazaliwa kwenye zizi na msichana na kutukuzwa na wachungaji wasiojulikana. Kila tukio kwenye simulizi la Luka linakwenda kinyume na matarajio, na hilo ndilo lengo. Anaonyesha jinsi Ufalme wa Mungu hufika mahali pasipo na hadhi––kwa wanaosubiri, wajane, maskini––kwa sababu Yesu yu hapa kuleta wokovu kwa kugeuza ukawaida wa mambo.

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com