Kugeuka kutoka kwenye mambo ya hisiaMfano
Moja kati ya ngome kubwa za hisia watu wanashughulika nazo leo inajukana kama kutegemea. Kuna majina mengine yanayopanua ngome hii kwenda zaidi ya uhusiano-- majina hayo yanweza kuwa kufurahisha watu na ulevi wa mitandao ya kijamii. Lakini, kwa wanaoanza, hebu tuangalie kutegemea.
Kutegemea ni utaratibu wa kuiga ( moja ya aina ya ngome za hisia) ambayo inamfanya mtu kushughulika-- mara nyingi kimakosa--na kukosa. Yawezekana kuna kukosa kujithamini mwenyewe na kujiheshimu au hisia kali ya kukataliwa. Pasipokujali, kutegemea mara nyingi kunahusisha kumtumia mtu au watu kurekebisha kilichovunjika. Naita hii kuwa na ngome ya watu.
Mungu pekee ndiye mwenye nguvu na uwezo kukutana na mahitaji yetu. Tatizo linakuja tunaposisitiza kuwageukia wengine kabla ya kumgeukia Mungu. Katika neno lake lote, tunasoma jinsi Mungu anavyowatumia watu katika maisha ya wengine. Hata hivyo, hakuna tunaposoma kwamba Mungu anapendezwa tunaporuhusu watu na vitu kuchukua nafasi yake. Ukweli, ni kwamba kinyume chake ni sahihi; tumeunda sanamu ya hisia. Hata ulevi wa mitandao ya kijamii unaweza kuingia kwenye kundi la ibada ya sanamu.
Kuna mstari mwembamba sana kati ya kufurahia uhusiano fulani au kufaidika kutokana na kuunganishwa kwenye mitandao ya kijamii na ugatuzi wa mahusiano ya hisia au ulinganifu. Watu na uhusiano ni zawadi ambayo tunatakiwa kufaidika. Lakini pia tunataka kuwa waangalifu kwamba hatutaki kuruhusu hisia zetu kugeuka kuwa ngome ya sonona, upweke, wivu, mashaka, au hofu.
Unahitaji kujikumbusha kwamba, katika Kristo, una kila kitu unachokihitaji. Huhitaji kushikilia kitu kutoka kwa watu fulani kukufanya ukamilike.
Nini au nani unamtegemea ili ujisikie wa thamani?
Tunatumanini mpango huu umekutia moyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma, bonyeza here.
Kuhusu Mpango huu
Wakati maisha yako hayako katika mpangilio na neno la Mungu ni dhahiri kabisa utapata matokeo ya kuumiza. Wakati hisia zako zonapokuwa hazina mpangilio na zinaanza kupanga maisha yako, unaweza kujikuta umejifungia katika gereza lako mwenyewe ambalo inaweza kuwa vigumu kutoroka. Unahitaji kutafuta uwiano sahihi na ujifunze kumwamini Mungu. Acha Tony Evans akuoneshe njia ya uhuru wa hisia.
More