Kugeuka kutoka kwenye mambo ya hisiaMfano
Hisia kwenye nafsi ni kama hisia kwenye mwili. Zinafunua jinsi tunavyojihisi kuhusu mazingira ya maisha yetu. Watu walioenda njia isiyo sahihi kwa hisia zao hujitahidi sana kuishi na wanaweza kujihisi hawana, msaada, tumaini, na thamani.
Ngome ya hisia haimaanishi kuwa na siku mbaya mara moja kwa muda. Ina maana ni wakati ambapo huwezi kukwepa mtego hasi ambao umeyafunga maisha yako, ikipelekea kuwa na kukata tamaa kusikodhibitiwa, huzuni, na uchungu.
Badala ya kufanya kitu watu wengine wanafanya ( ambacho ni kujaribu kukataa au kupuuzia kifungo cha hisia kwa kunywa dawa, burudani, ngono, au kutumia fedha), nataka nikusaidie kugundua kiini cha unayopitia ili uweze kushinda. Ukweli ni kwamba Mungu hakukuumba kubeba ngome za hisia kwa miaka, mitano, ishirini, au arobaini, au muda wowote.
Badala yake, Mungu amekuahidi, katika Kristo, maisha makamilifu. Yesu alisema, “ mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”(Yn 10:10)
Hajakuita kuishi kila siku kwa kushindwa. Anataka ujue na uamini kwamba yeye ndiye anayetawala, na kwamba anakuangalia maisha yako yote. Kama hupati maisha kamili anayotoa Yesu bure, ni wakati wa kugeuka. Mgeukie Mungu, muombe akufunulie maeneo unayokosa imani na ambapo ngome ya hisia inaweza kuwa imejengwa. Anataka kukusaidia kujifunza kuona mbali zaidi ya huzuni zako--kuyaangalia maisha yako kama yeye anavyoyaona. Anaweza kufanya muujiza kutoka kwenye kitu kinachoonekana kimeharibika.Kuna hisia ambazo zinaonekana kuwa na ngome maishani mwako? Uko tayari kuzikabidhi kwa Mungu?
Kuhusu Mpango huu
Wakati maisha yako hayako katika mpangilio na neno la Mungu ni dhahiri kabisa utapata matokeo ya kuumiza. Wakati hisia zako zonapokuwa hazina mpangilio na zinaanza kupanga maisha yako, unaweza kujikuta umejifungia katika gereza lako mwenyewe ambalo inaweza kuwa vigumu kutoroka. Unahitaji kutafuta uwiano sahihi na ujifunze kumwamini Mungu. Acha Tony Evans akuoneshe njia ya uhuru wa hisia.
More