Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kugeuka kutoka kwenye mambo ya hisiaMfano

A U-Turn From Emotional Issues

SIKU 2 YA 3

Ngoja nikukumbushe ukweli muhimu kuhusu hisia: hazina akili. 

Hazifikirii. Zinaitikia tuu. Hisia lazima ziazime mawazo ili kuamsha kujisikia. Kwa hiyo, yeyote au chochote kinachoongoza mawazo yako, huongoza unavyojisikia. Hisia zako zinajengwa na kutawaliwa na unavyofikiri kuhusu mambo fulani katika maisha yako. Kwa hiyo, kama unataka kuthibiti hisia zako na kushinda ngome ya hisia katika maisha yako, unahitaji kuthibiti kufikiri kwako.

Unapopangilia mawazo yako na kweli ya Mungu, utawekwa huru.

Hebu jiangalie kwenye kioo. Mtu huyo unayemuona alisulubiwa pamoja, alizikwa pamoja, na kufufuka pamoja na Kristo. Machoni pa Mungu, wakati Yesu alipokufa zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita, na wewe pia. Alipozikwa, ulilala kaburini pamoja naye. Alipofufuka, ulifufuka pia. Hata kama unaweza kuwa umempokea Kristo siku chache zilizopita, Mungu alichukua kilichotokea kwa Yesu miaka mingi iliyopita na kukifanya sehemu ya ukweli wako wa kiroho.

Shetani ni bwana wa kupanda mawazo katika akili yako na kukufanya ufikirie ni ya kwako. Yawezekana unamsikia akisema kitu kama, " siwezi kushinda kudharaulika na mtego wa kulinganishwa. Siwezi kuwa huru kutoka katika kifungo hiki cha hisia. Ziwezi kuzipinga tabia hizi za zamani za kuangukia kwenye sonona." Anaweza kukwambia mambo hayo, au unaweza kujiambia mwenyewe, lakini ili uyashinde, lazima uache kuamini uongo. Mawazo yote hayo yangeweza kuwa kweli wakati utu wako wa kale ulikuwa hai, lakini utu huo ulikufa msalabani pamoja na Kristo. Wewe ni kiumbe kipya kabisa (2 Wakorintho 5:17).

Ni uongo gani unaouamini kuhusu wewe?

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

A U-Turn From Emotional Issues

Wakati maisha yako hayako katika mpangilio na neno la Mungu ni dhahiri kabisa utapata matokeo ya kuumiza. Wakati hisia zako zonapokuwa hazina mpangilio na zinaanza kupanga maisha yako, unaweza kujikuta umejifungia katika...

More

Tunapenda kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha