Kugeuka na Kurudi Upande wa Pili Kutoka UraibuMfano
Unapomruhusu Roho atawale mawazo yako kwa ukweli wa Neno la Mungu, utaishi huru. Kama Yesu alivyosema, “mtajua ukweli, na ukweli utawaweka huru” (Yohana 8:32). Neno “jua” lina maana zaidi ya utambuzi wa kiakili wa jambo. Maana yake ni kuwa na uhakika wa kina bila mashaka kuhusu jambo. “Unajua kwamba unajua” ni kweli. Ni ukweli ambao unaafikiana na kiini chako. Hii ndiyo maana ya kujua ukweli na kuwekwa huru.
Aina hii ya “ujuzi” ambayo Yesu anaongelelea ambao utakuweka huru ni ujuzi ambao hakika unajua. Si kukisia. Si kutumaini. Si jaribio. Unajua kwamba unajua kwa sababu umepitia na kupata kwamba ni kweli.
Lakini katika Neno la Mungu, si kila mara tunapata ithibati ya kuaminika kabla ya kupata imani inayohitajika kufanya kazi ya ukweli. Hii ndio maana imani katika neno la Mungu linabeba uzito mkuu na ni muhimu sana katika mchakato wa kushinda tabia za kiraibu. Sharti uamini kwamba Neno la Mungu ni kweli, kisha ulitumie katika hali yako kama ukweli ili iafikiane na ifanye kazi yake maishani mwako ya kukuweka huru. Ukweli unakusaidia kushinda ngome zako, ikiwa utauchukua kuwa ukweli. Lazima ufangamane akili yako, matendo yako, moyo wako na hiari yako pamoja na Neno la Mungu na utawala wake kuhusu hali au mfululizo wa mawazo wowote unaopitia ili likuweke huru.
Ni nini kutoka Neno la Mungu unayojua ambayo inaweza kukusaidia kupata uhuru kutokana na uraibu?
Tunatumai mpango huu ulikuhamasisha. Kwa maelezo zaidi kuhusu kugeuka na kurudi upande ulikotoka katika maisha yako, bofya hapa.
Kuhusu Mpango huu
Ikiwa maisha yako hayako katika mpangilio na Neno la Mungu, hakika utapatwa na matokeo machungu. Wengi wamepambana na afya yao, kupoteza ajira, na mahusiano, na kujipata kwamba wanahisi kwamba wapo mbali na Mungu kwa sababu ya uraibu. Inaweza kuwa uraibu wenye uzito kama vile mihadarati au ponografia ama uraibu ndogo, kama chakula ama burudani, uraibu unavuruga maisha yetu. Mruhusu mwandishi mashuhuri Tony Evans akuonyesha njia ya uhuru.
More