Kugeuka na Kurudi Upande wa Pili Kutoka UraibuMfano
Sababu moja ambayo inafanya watu wakwame katika uraibu wao ni kwamba wanakita msingi wa mtazamo wa mawazo yao katika uongo. Uongo mmoja mkuu unaochangia uraibu ni kwamba unaweza kurekebisha mwili kwa kutumia mwili. Lakini Paul anatuambia katika 2 Wakorintho 10; hatupigani kwa jinsi ya mwili. Mwili hauwezi kurekebisha mwili. Ndio, unaweza kujaribu kuudhibiti, na huenda utafanikiwa kwa muda. Lakini daima huwezi kurekebisha shida ya dhambi kwa kutumia mwili wako wenye dhambi kama tiba. Unachofaa kufanya ni kuenda kwa ukweli wa Neno la Mungu kwanza. Ukweli wake utakuachilia huru. Ukweli wake unapenya na kuleta uzima. Ukweli wake unafumua maongo ambayo yamekufunga katika msongo wa mateso na yanayokunasa katika dhambi na matokeo yake.
Kujaribu kujiondoa kutoka ngome ya dhambi kupitia nguvu zako mwenyewe ni kama wanawake wa kale walioosha nguo kwa kutumia ubao. Ilichukua siku kadhaa kuziosha, na bado, nguo hazikung'ara hata baada ya juhudi nyingi. Nguo zilichakaa na dobi pia alichoka, akaumia, na kufadhaika. Mungu ametupa suluhu ya dhambi kupitia mwosho wa wokovu uliotolewa na Mwanawe. Dhabihu ya Yesu inatupa fursa ya kutumia nguvu ya Roho aliye ndani yetu. Roho anatuwezesha kutambua na kupokea ukweli (Yohana 16:7-11). Roho anatusaidia tutende alivyotuamuru Yesu katika Yohana 8, yaani “kukaa katika Neno lake.” Neno “kukaa” lina maana ya kushiriki, kushinda mahali—kubaki. Lazima ubaki katika ukweli, wala si kuutembelea pekee.
Je, umefanikiwa katika juhudi zako za kimwili kushinda uraibu wako? Mkakati bora zaidi ni upi?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Ikiwa maisha yako hayako katika mpangilio na Neno la Mungu, hakika utapatwa na matokeo machungu. Wengi wamepambana na afya yao, kupoteza ajira, na mahusiano, na kujipata kwamba wanahisi kwamba wapo mbali na Mungu kwa sababu ya uraibu. Inaweza kuwa uraibu wenye uzito kama vile mihadarati au ponografia ama uraibu ndogo, kama chakula ama burudani, uraibu unavuruga maisha yetu. Mruhusu mwandishi mashuhuri Tony Evans akuonyesha njia ya uhuru.
More