Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kugeuka na Kurudi Upande wa Pili Kutoka UraibuMfano

A U-Turn From Addiction

SIKU 1 YA 3

Watoto wengi wa Mungu ni mateka wa kiroho. Wamenaswa katika mzunguko wa dhambi ambao hawajaweza kuvunja. Haijalishi iwapo ni ulevi, uyakinifu, machungu, wivu, ulafi, kujihurumia, ponografia, mihadarati, michezo mtandaoni, matusi, mitandao ya kijamii, kujidunisha, hasira, ama chuki—uraibu wa mitindo ya kihisia au kikemikali unafunga watu wengi sana leo. 

Neno la kibiblia la dhana ambalo tunaijua leo kuwa uraibu ni ngome. Uraibu, ama dhana sahihi zaidi—ngome ya kiroho, ni mtazamo ya mawazo na matendo uliopigwa chale akilini mwetu. Tunasadiki na kuendeleza shughuli zetu kana kwamba hali yetu haliwezi kubadilika, ingawa ni kinyume na matakwa ya Mungu. Tunakuwa watumwa wa dhambi na inatawala fikra zetu, maamuzi yetu, na matendo yetu. 

Hatua ya kwanza ya kugeuza uraibu ni kutaka kuachiliwa huru. Yesu aliwauliza watu iwapo walitaka wawe wazima (Yohana 5:6). Ikiwa mtu amekwama na anataka kubaki alipokwama, hakuna kitu ambayo yeyote anaweza kufanya ili waendelee katika mwelekeo unaofaa. Sharti uhuru kutokana na tabia za kiraibu uanze ndani. Ukijipata umetegwa na uraibu na kushawishwa na mtazamo hasi wa fikra, unaweza kuhisi kana kwamba nyoka amejikunja akilini mwako. 

Huu ni wakati wa kuchagua mwelekeo mpya wa uhuru. Unhuru unaanza na kuchagua kutoka njia yako ya sasa na kuelekea mwelekeo tofauti. 

Kwa kweli, u tayari kuaga uraibu wako na kumruhusu Yesu akuachilie huru?

siku 2

Kuhusu Mpango huu

A U-Turn From Addiction

Ikiwa maisha yako hayako katika mpangilio na Neno la Mungu, hakika utapatwa na matokeo machungu. Wengi wamepambana na afya yao, kupoteza ajira, na mahusiano, na kujipata kwamba wanahisi kwamba wapo mbali na Mungu kwa sababu ya uraibu. Inaweza kuwa uraibu wenye uzito kama vile mihadarati au ponografia ama uraibu ndogo, kama chakula ama burudani, uraibu unavuruga maisha yetu. Mruhusu mwandishi mashuhuri Tony Evans akuonyesha njia ya uhuru.

More

Tunapenda kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/