Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hatua Zako za MwanzoMfano

Your First Steps

SIKU 5 YA 5

JUMUIYA

Hauko peke yako katika hili.

Umeafanya maamuzi ya kuishi aina mpya ya maisha--yaisha ya kujitoa kumfuata Yesu, na hayo yanaweza kuonekana magumu sana.

Na ni kweli.

Lakini hauko peke yako.

Kwanza, Yesu hatakuacha. Yeye amejitoa kikamilifu kwako, na hawezi kamwe kurudi nyuma katika kujitoa huko.

Na pili, Yesu hajakualika tuu katika maisha mapya, bali katika familia mpya. Anakupa jumuiya mpya kabisa kuungana nao. Tunaiita Kanisa.

Na kamisa linaweza kuwa chafu kwa sababu watu ni wa chafu.

Na kanisa linaweza kuwa dhaifu kwa sababu watu ni wadhaifu.

Na kanisa linaweza kuwa zuri kwa sababu watu ni wazuri.

Wakati kanisa linapokuwa katika ubora wake, ni la miujiza--koloni la mbinguni hapa duniani. Tunatiana moyo, na kuinuana kukua tunapomfuata Yesu. Kila mmoja anawajibika, na kwa upendo kumwongoza kila mmoja mbali na tabia zinazoharibu na mienendo na kumrejesha kwenye njia za Yesu.

Jiunge na kanisa; jihusishe. Usitegemee ukamilifu kwa sababu hata hivyo, wewe si mkamilifu.

Lakini kama ni kanisa linalosimama na Yesu na limejitoa kuishi kufuata njia zake kwa majirani, basi ni familia unayostahili kujiunga nayo.

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Your First Steps

Umefanya uamuzi wa kumfuata Yesu, sasa nini kinafuata? Mpango huu si orodha kamili ya kila kitu kinachokuja kutokana na uamuzi huo, lakini utakusaidia kuchukua hatua zako za kwanza.

More

Tunapenda kuwashukuru SoCal Youth Ministries - AG kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea visit: http://youth.socalnetwork.org