Hatua Zako za MwanzoMfano
MPYA
Nilipokuwa darasa la nne, nilikuwa kwenye orodha ya shule nzima ya wahitimu wa Jiographia. Ni sahihi, shule yangu haikuwa na sifa kubwa kwenye kusoma. Mimi nilikuwa katika tatu bora. Ndipo, swali langu likaja. Swali gumu nililolipata kwa siku zote.
Na nililikosa.
Kibaya zaidi, nilijua majibu ya maswali mawili yaliyofuata, maswali yaliyoamua nani wa nafasi ya kwanza, na wa pili. Kama maswali yangeulizwa katika namna tofauti kidogo, ningeshinda.
Sikuwahi kutamani nafasi ya pili kama nilivyofanya siku ile.
Kwa kuamua kumfuata Yesu, unapata zaidi ya nafasi ya pili, unapata maisha mapya kabisa.
Unapochagua kumfuata, maisha yako ya kale yanaondoka, na maisha mapya yanaanza.
Siyo nafasi ya pili tuu--maisha mapya.
Hiyo ina maanisha hutakiwi kushughulika na athari za maamuzi ya kale? Hapana, lakini haimaanishi aina mpya yako, na asili mpya, sasa vina nafasi kusonga mbele.
Unapochukua hatua za mwanzo katika kumfuata Yesu kunakufanya wewe kuwa mtu mpya kabisa. Pokea utambulisho mpya, furahia maisha mapya, na uyatumie kuuonesha ulimwengu kwamba Yesu ni bora kuliko nafasi ya pili.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Umefanya uamuzi wa kumfuata Yesu, sasa nini kinafuata? Mpango huu si orodha kamili ya kila kitu kinachokuja kutokana na uamuzi huo, lakini utakusaidia kuchukua hatua zako za kwanza.
More