Hatua Zako za MwanzoMfano
SOMA
Kuna zaidi, inaonekana kama kuna mawazo mengi kuliko watu waliopo. Na mawazo yote hayo yanaendelea kuhama na kubadirika. Kusema kweli, inaweza kuwa ngumu sana kwenda sambamba.
Mabadiriko ya desturi yanaleta swali, "Ukweli ni nini?"
Kama utamfuata Yesu, basi utahitaji kuweka nanga maisha yako kwenye kweli. Hii ni moja ya sababu zinazowafanya wakristo tofauti na watu wengine ambao hawamfuati Yesu: tunakabidhi maisha yetu ili tuishi katika kweli ya maandiko. Sisi siyo watu wa kuyumbishwa na maoni; badala yake tunajitahidi kuyaleta maisha yetu kwenye kuendana na kile ambacho Biblia inafundisha.
Na kuna njia moja tuu ya kufanya hilo:
Soma.
Sikiliza.
Jifunze.
Kama tutamfuata Yesu, yatupasa kuyajua mafundisho ya maandiko, ndipo kuyaleta maisha yetu kuendana na yanayotufundisha. Tunapaswa kuishi kufuatana na maandiko, na siyo kufuata utamaduni.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Umefanya uamuzi wa kumfuata Yesu, sasa nini kinafuata? Mpango huu si orodha kamili ya kila kitu kinachokuja kutokana na uamuzi huo, lakini utakusaidia kuchukua hatua zako za kwanza.
More