Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Mungu ni MTAKATIFU. Aliwapa amri ili wajifunze utii (2:17, Matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika). Amri mojatu! Lakini wakaanguka. Kwa kutokutii wamejitenga na Mungu. Wamejitenga na uhai, maana Mungu ndiye asili ya uhai wao. Hakika watakufa kama Mungu alivyosema. Tena wamelaaniwa, kwa hiyo hata muda watakaoishi utakuwa wa taabu (m.16-19). Lakini UPENDO wa Mungu unaonekana pia! Akawavika mavazi ya ngozi (m.21) na akatoa ahadi ya ukombozi: Nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino(m.15). Huu ni unabii wa kwanza juu ya Kristo! Zingatia Agano Jipya linavyosema: Kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa(Ebr 2:14-15). Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi(1 Yoh 3:8).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz