Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la BWANA(4:26). Mungu hakuendelea kuwatembelea watu na kusema nao kama huko bustanini, na kama alivyokuja kwa Kaini (4:6-7 na 9-12). Ndipo wakaanza kuomba na kuabudu, maana BWANA hakuonekana tena machoni pao. Ni kama ilivyo sasa baada ya Yesu kupaa. Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka(Rum 10:13). Jina hili BWANAni takatifu kwa Waisraeli. Kwa Kiebrania limeandikwa kifupi: YHWH. Waliogopa hata kulitamka. Kisha matamshi yake yakasahaulika. Huenda ni YAHWEH.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz