Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

SIKU 29 YA 31

Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo(m.11). Fikiria! Maneno haya yameandikwa na mtume Petro ambaye kwanza hakuelewa kabisa haya, bali alitaka kumzuia Yesu asipate mateso! (Mt 16:21-23, Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu). Sasa Petro amefundishwa na Yesu (Lk 24:44-49, Yesu akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya). Pia Roho Mtakatifu amemkumbusha Petro (katika Yn 16:13-14 Yesu anasema, Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari). Ameona kwamba bila mateso ya Yesu, wokovu usingalipatikana (m.2)! Ameelewa maneno ya nabii Isaya kuhusu Yesu: Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote(53:4-6)!

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz