Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Nyoka alinidanganya, nikala(m.13). Shetani alikuja kwa sura ya nyoka (Ufu 12:9, Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote). Naomba ujifunze jambo moja muhimu: Shetani siku zote hutumia udanganyifuili kumpata mwanadamu! Anayafanya yaliyo kinyume cha mapenzi ya Mungu kuonekana kuwa ni kitu chema cha kutamani (m.6,Mwanamke aliona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa). Shetani hugeuza Neno la Mungu kidogotu ili usitambue kuwa anakudanganya: "miti yote"(m.1). Hawa naye akageuza kidogo: "wala msiyaguse"(m.2). Ndipo Shetani akasema uongo mtupu: Hakika hamtakufa (m.4), maana Mungu alikuwa amesema: Matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika(2:17)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz