Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuamini Mungu ni vyema Bila kujali loloteMfano

Believing God Is Good No Matter What

SIKU 3 YA 5

"Kuwa Mtafutaji wa Mema"

Kutafuta wema wa Mungu kila siku husaidia kutarajia mema maishani mwetu. Wema wa Mungu haujifichi, na fadhili zake hazina kikomo... twahitajika kuwa na macho ambayo yanatafuta kupata. Huwa hatuna ufahamu wa fadhili za Mungu, ndio maana Mtume Paulo aliwaombea marafiki zake wawe na ufahamu.

Paulo aliandikia kanisa la Efeso na akawaambia kuwa anaombea macho yao ya moyo yapate ufahamu." Mpango ni huu: Fadhili zimetuzunguka. Wakati ninapoanza kutafuta vitu vyema maishani mwangu, Mimi hutambua kuwa vinapatikana kila mahali hata nisipotarajia. Wakati fadhili za bwana hazionekani, zinawezakuwa zinafanya kazi nzuri kwa niaba yetu. Funza macho yako kuona mema na kutazama wema ambao umeonyeshwa kila mahali.

Fadhili za Mungu zinaweza kuvutwa upande wako kulingana na mtazamo wako na mawazo yako na zinaweza kuzuiliwa vile vile na mtazamo na mawazo yako. Fadhili zinaweza kuwa bila upendeleo kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, lakini haimaanishi kuwa ni sambamba na mtazamo na mawazo za kila mtu. Tukiamua kuwa watafutaji mema, hilo linaongeza fadhili za Mungu maishani mwetu.

Hembu fikiria: Ni vipi unaweza kufundisha tena mawazo yako kulenga na kuzingatia mambo mazuri?

MAOMBI: Asante Mungu kwa kunipa uwezo wa kufundisha tena mawazo yangu ili nione mengi mazuri ambayo ni sehemu ya misha yangu. Nataka kuwa mtafutaji wa mambo mema ili mradi niweze fikiria na kutarajia mengi ya fadhili zako kila siku. Katika jina La Yesu. Amina.
siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Believing God Is Good No Matter What

Kuna jumbe fulani siku hizi, nje na ndani ya Kanisa, ambazo zimepaka tope ujumbe wa kweli wa fadhili za Mungu. Ukweli ni kwamba, Mungu hashurutishwi kutupea vitu vizuri—lakini anataka! Siku tano zijazo zitakusaidia kuangalia upya kando yako kwa macho yanayoona vitu vinavyokupotosha kila siku na kuona wema chungu nzima wa Mungu.

More

Tungependa kushukuru kikundi cha uchapishaji cha WaterBrook kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.goodthingsbook.com