Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuamini Mungu ni vyema Bila kujali loloteMfano

Believing God Is Good No Matter What

SIKU 1 YA 5

"Hakuna wema ila Mungu."

Watu wengine hudhani Mungu ni mwenye hasira mara nyingi na kuwa fadhili zake hudumu kwa muda tu, lakini Biblia inatuambia kuwa hicho ni kinyume. Wewe ni mpendwa wake hata kama unahisi kama wewe ni mtu mbaya.

Mungu amesonga mbele kutoka kwa hilo jambo mbaya ulilolifanya au hicho kitu kibaya ulichokisema. Inawezekana alikuwa na hasira au alisikitishwa wakati huo, lakini amesonga mbele. Je wewe? Haufai kuwa na wasiwasi kuhusu kupotea kutoka kwa fadhili za mungu kwa sababu ya kushindwa.

Wema wa Mungu unaendelea na kamwe hauishi. Fadhili zake daima ziko nasi; Fadhili za Mungu ni za milele!

Kwa kweli, wema haupo bila Mungu; wema haukutokea peke yake—mbali au kando ya Mungu. Ni dhahiri sio kitu kinachotokana na wanadamu (Je, unahitaji kuwafunza watoto wako kuwa wazuri au wabaya?)

Mungu ni chanzo cha mema na vitu vyote vyema. Watu wengine bado wanatenganisha Mungu na wema. Hili jambo linaweza zorotesha uhusiano wa mwanadamu wa kumshukuru, kumheshimu na kumwabudu Mungu.

Somo hili ni kuhusu safari ya kuanza kufunza macho zako kuona wema wa Mungu ambao hauonekani na fadhili zake katika maisha yako ya kila siku. Kwa siku tano zijazo utaanza kuona maisha yako kupitia fadhili za Mungu.

Hembu fikiria: Ni mambo yepi mazuri maishani mwako ambayo ni rahisi kutoyaona?

OMBI: Mungu, asante kwa kuwa kwa maisha yangu sasa. Nisaidie niyafungue macho yangu nakuona kuwa wewe ndio chanzo cha vitu vyote vyema na kuwa unaleta fadhili maishani mwangu kila siku. Katika jina la Yesu. Amina.


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Believing God Is Good No Matter What

Kuna jumbe fulani siku hizi, nje na ndani ya Kanisa, ambazo zimepaka tope ujumbe wa kweli wa fadhili za Mungu. Ukweli ni kwamba, Mungu hashurutishwi kutupea vitu vizuri—lakini anataka! Siku tano zijazo zitakusaidia kuangalia upya kando yako kwa macho yanayoona vitu vinavyokupotosha kila siku na kuona wema chungu nzima wa Mungu.

More

Tungependa kushukuru kikundi cha uchapishaji cha WaterBrook kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.goodthingsbook.com