Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuamini Mungu ni vyema Bila kujali loloteMfano

Believing God Is Good No Matter What

SIKU 2 YA 5

"Fadhili za Familia"

Fadhili za Mungu hutiririka kikawaida maishani mwetu kama vile fadhili za baba hutiririka maishani mwa watoto wake. (Na yeye ni ni Picha kubwa ya baba unayoweza ota au fikiria.) Mungu anakupenda. Anakuchukua kama mtoto wake, na hilo linakufanya kuwa mmoja wa kizazi cha kupokea baraka zake.

Usihisi kama unahitajika kuomba msamaha kwa watu, au kuhalalisha wema wa Mungu kwa wale ambao hawaelewi au hawakubali. Kuna watu daima wanangoja kukosoa ushindi wako au kupuuza baraka zako, kwa sababu walihisi kuwa mtu mwingine alistahili zaidi. Kwa kweli, kama ushawahi hisi kwamba mtu fulani hastahili baraka ambayo amepokea (Sisi sote tunafahamu haya.. .), pengine ni ukweli! Lakini huu hapa muda wa ukweli kwetu sisi sote: hatuwezi chukia fadhili katika maisha ya mtu mwingine ikiwa tutakaribisha fadhili hizo maishani mwetu.

Tunapoanza kuelewa kuwa fadhili hizo ni dhihirisho la neema ya Mungu, basi tunaweza tukaelewa kuwa fadhili hizo tumepokea—kama neema—hatustahili kupokea.

Hembu fikiria: Ni mifano ipi maishani mwako ambapo ulipokea fadhili zisizotarajiwa ambazo hukustahili kupata?

OMBI: Mungu, asante kwa kuwa Baba kwangu, Haijalishi babangu wa dunia amekuaje, wewe ni baba mkarimu na una fadhili zisizoisha ghalani kwa sababu ya maisha yangu ya baadaye. Nifundishe leo kukubali fadhili za familia ambazo umeniwekea kama mtoto wako. Katika jina la Yesu Kristo. Amina.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Believing God Is Good No Matter What

Kuna jumbe fulani siku hizi, nje na ndani ya Kanisa, ambazo zimepaka tope ujumbe wa kweli wa fadhili za Mungu. Ukweli ni kwamba, Mungu hashurutishwi kutupea vitu vizuri—lakini anataka! Siku tano zijazo zitakusaidia kuangalia upya kando yako kwa macho yanayoona vitu vinavyokupotosha kila siku na kuona wema chungu nzima wa Mungu.

More

Tungependa kushukuru kikundi cha uchapishaji cha WaterBrook kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.goodthingsbook.com