SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano
![SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F17940%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Amri ya sita inasema, “Usizini”. Yesu anatoa mkazo juu ya amri hii kwamba isitazamwe katika hali ya nje tu, maana uovu huanzia ndani ya moyo wa mtu. Wakati wa Musa kulikuwa na tatizo la maisha ya ndoa. Hali hiyo ikapelekea kuruhusu mume kumpa talaka mke wake. Biblia inasema Musa alifanya hivi kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu. Huo haukuwa mpango wa Mungu. Tukisoma Mk 10:6-12 tunapata mafundisho ya ndoa ya Kikristo kwa mpango wa Mungu: Tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo. Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake; na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini. Kwa hiyo, wanandoa na watakaoingia katika ndoa baadaye wanapaswa kuishi kulingana na Neno la Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F17940%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana
![Soma Biblia Kila Siku Julai 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26577%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021
![Upendo Wa Bure](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26579%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Upendo Wa Bure
![Soma Biblia Kila Siku Februari 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F23985%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Februari 2021
![Soma Biblia Kila Siku Mei 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F25588%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Mei 2021
![Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26578%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?
![Soma Biblia Kila Siku 11/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F22531%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/2020
![BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F24935%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo
![Soma Biblia Kila Siku Januari 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F23329%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Januari 2021
![Soma Biblia Kila Siku Machi 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F24503%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Machi 2021
![Moyo - Neno La Mungu Hugeuza Moyo](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F22660%2F320x180.jpg&w=640&q=75)