SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano

Lengo la Mungu kuwakomboa Waisraeli kutoka utumwani Misri lilikuwa ni kuwarudisha kwake. Kwao ni kule ambako Mungu alikusudia waweko tangu asili. Mungu anataka warudi huko. Asili yao ni kwa Mungu, kama Mungu mwenyewe anavyowakumbusha katika m.4,Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. Pale alipo Mungu, ndipo anapenda na watu wake wawepo. Upekee wa taifa la Mungu unaonekana pale tu wanaposikiliza maagizo ya Mungu na kuyafuata. Taifa la Israeli linawakilisha mataifa yote ya dunia. Uteule huu unaambatana na kuwajibika na kuishi kwa kufuata utakatifu wa Mungu: Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. … ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu(1 Pet 2:5 na 9).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021
