Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10

SIKU 13 YA 31

Bwana ni nguvu ya watu wake, maana kwao ni mwamba(m.1), ngao(m.7) na ngome ya wokovu(m.8), yaani mahali pa kukimbilia ili wasife. Hili ni hitimisho la Mwimba Zaburi juu ya msaada wa Mungu kwa wanaomtumainia. Yeye mwenyewe alipomwita Mungu na kuomba msaada wake, alisikilizwa: Ameisikia sauti ya dua yangu(m.6). Mungu huwapatiliza waovu sawasawa na uovu wao, naye atawavunja wala hatawajenga(m.5). Lakini Mungu hawanyamalii wamwitao, wala hawajumlishi wamtumainiao pamoja na wasio haki. Je, wewe unatumania na kutegemea nini katika maisha yako? Tafakari m.7, na fanya kama Mwimba Zaburi: Mtumainie Mungu! Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, nami nimesaidiwa; basi, moyo wangu unashangilia, na kwa wimbo wangu nitamshukuru.

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz