Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 7 YA 30

Ni ajabu! Baraka zile zilizotajwa jana, Waisraeli hawakupokea kwa moyo wa shukrani na unyenyekevu mbele za Bwana. Badala yake walizipokea kwa kiburi na kaidi (m.15: Yeshuruni[= jina la heshima kwa Israeli] alinenepa, akapiga teke; umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, akamdharau Mwamba wa wokovu wake) na kuiabudu miungu batili (m.16-17: Wakamtia wivu [Bwana]kwa miungu migeni, wakamkasirisha kwa machukizo. Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, kwa miungu wasiyoijua, kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, ambayo baba zenu hawakuiogopa). Bwana alichukizwa sana na tendo hilo na kutaka kuwafutia mbali. Ila hakufanya hivyo, maana alijua kwamba mataifa yataanza kujidai kuwa miungu yao ni yenye nguvu kuliko Mungu wa Israeli (m.27: Naliogopa makamio ya adui, Adui zao wasije wakafikiri uongo, Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka, Wala Bwana hakuyafanya haya yote). Je, wewe ndugu, Waudharau wingi wa wema wake … usijue kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? (Rum 2:4).

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz