Soma Biblia Kila Siku 9Mfano
Basi ikawa hapo Musa alipomaliza kuandika maneno ya torati hii katika chuo, hata yakaisha(m.24). Maneno haya yanathibitisha kwamba Musa ndiye mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati na hata vitabu vile vinne vinavyotangulia, yaani, kitabu cha Mwanzo hadi kitabu cha Hesabu (taz. pia m.9: Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi). Kuanzia hapo Neno la Mungu lilikuwa linaambatana na taifa la Israeli kwa karibu (m.26: Twaeni chuo hiki cha torati, mkiweke kando ya sanduku la agano la Bwana, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako). Sisi Wakristo tusio Wayahudi tuna deni kubwa kwa taifa la Israeli, maana wao wamekabidhiwa mausia ya Mungu(Rum 3:2). Wameyatunza kwa uangalifu mpaka sisi tukayapata.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz