Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 3 YA 30

Musa amefika umri wa miaka 120 (m.2: Musa akawaambia [Waisraeli], Mimi leo ni mwenye miaka mia na ishirini). Miaka hii inaweza kugawanyika katika awamu tatu zifuatazo: Miaka 40 alikuwa huko Misri (Mdo 7:21-23: Binti Farao akamtwaa[Musa], akamlea awe kama mwanawe. Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo. Umri wake ulipopata kama miaka arobaini akaazimu moyoni mwake kwenda kuwatazama ndugu zake Waisraeli), miaka 40 alikuwa mchunga kondoo Midiani (Mdo 7:30: Hata miaka arobaini ilipotimia, malaika wa Bwana akamtokea[Musa] katika jangwa la mlima wa Sinai katika mwali wa moto, kijitini), na mwisho alipata kulitumikia taifa la Israeli miaka 40. Sasa anaelekea kustafu, na anataka Waisraeli wakumbushwe kuwa Yoshua ndiye kiongozi wao mpya (m.3: Yoshua atavuka mbele yako, kama Bwana alivyonena). Wote anawatia moyo kwa kuwakumbusha kwamba BWANA atavuka pamoja nao na kuwapa ushindi. Bwana hastafu wala kupungukiwa nguvu. Hadi leo Bwana ni yeye yule. 

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz