Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kwa pamoja: Kutafuta maisha pamojaMfano

Collective: Finding Life Together

SIKU 7 YA 7

Lini unajisikia kama mtu mzima au unataka kutulia

Umefika siku ya mwisho ya mpango huu wa Biblia, lakini yawezekana bado una maswali mengi kuliko majibu. Hiki ndiyo unachotakiwa kukijua: Ni sawa.

Huwezi kuanza kujisikia kama wewe ni mtu mzima, na hujisikii kama una majibu yote. Na hivyo ndivyo Mungu alivyoumba. Kama tungekuwa na majibu yote, tusingemhitaji Mungu.

Zaburi 119:105 inatuambia kwamba Neno la Mungu ni taa ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu. Ni taswira nzuri. Kimsingi, inatuambia kwamba Mungu anatupa taarifa za kutosha ili tufanye kwa usahihi kitu kinachofuata. Lakini hatuoni taswira kamili. Na huo ndiyo ukweli. Kwa sababu hatujui kinachofuata, ni fursa ya kumwamini Mungu.

Tunaweza kumkaribia Mungu na jinsi tunavyofikiria maisha yetu yanavyoweza kuonekana, lakini mipango yetu inakuwa wazi tukijua kwamba makusudi ya Mungu ni bora zaidi kuliko tunavyoweza kuomba, kufikiria, au kuwaza.

Kwa hiyo usijisumbue sana kujaribu kuyaweka maisha yako sawa. Alama ya kweli tabia siyo kitu kikubwa unachokifanya kwamajili ya kazi yako. Ni jinsi unavyompenda jirani yako vyema. Tumia karama za Mungu alizoweka ndani yako kuubadili ulimwengu mbele yako.

Usijali ni kwa jinsi gani hujui. 1 Korintho 8:1 inatukumbusha kwamba ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga kanisa. Baadhi ya maneno ya mwisho ya Yesu yalikuwa katika maombi kwa Mungu kwamba tuishi kwa umoja. Hii inatuambia kwamba maoni yetu si bora kuliko upendo wetu kati yetu.

Kuwa mtu mzima si kufikia hatua fulani. Ni kujifunza jinsi ya kumtegemea Mungu na wanaokuzunguka. Kaa katika neno la Mungu. Fanya lililojema analokutaka ulifanye. Utakapofanya hivyo? Litakujenga na kulijenga kanisa.

Fikiria: Ni njia zipi unaweza kujifunza kumtegemea Mungu zaidi na wanaokuzunguka? 

Omba: Mungu, asante kwa ajili ya mipango uliyonayo kwa ajili yangu. Nisaidie kushika mipango hiyo kwa mikono iliyowazi, nikiamini kwamba kusudi lako ni zaidi ya navyoweza kuomba, fikiria au kuwaza. Nizungukwe na watu sahihi. Nisaidie kufanya kile unachoniita nifanye. Nisaidie kukupenda na kuwapenda wengine kila siku. Katika jina la Yesu. Amen. 

Pata dondoo za utu uzima kutoka finds.life. 

siku 6

Kuhusu Mpango huu

Collective: Finding Life Together

Unapofikia umri wa miaka 18, unaanza kuona kwamba unahitaji kupanga maisha yako. Itakuwaje usipofanya hivyo? Itakuwa kama ulipofikiria utakuwa sipo ulipo sasa? Hauko peke yako. Hebu tuangalie swali kuu la maisha yetu pamoja katika mpango huu wa Biblia wa siku 7 kwa pamoja, mafunzo ya vijana kutoka Life. Church.

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/