Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kwa pamoja: Kutafuta maisha pamojaMfano

Collective: Finding Life Together

SIKU 3 YA 7

Nawapataje marafiki?

Tumeona kwamba kuwapata marafiki ni jambo la muhimu ili kupata mwelekeo katika maisha yetu. Lakini kutafuta marafiki kama mtu mzima inaweza kuonekana kitu cha aibu. Sasa, unatafutaje watu wako?

Kwanza kabisa, jua kwamba Mungu ni mwaminifu kukupatia 1 Yohana 5:14 inasema tunaweza kuwa na ujasiri kwamba Mungu anatusikia tuombacho chochote kinachompendeza. Kuwa na watu wakuishi nao ni sehemu ya mpango wa Mungu kwa ajili yetu. Kwa hiyo, tunaweza kuwa na ujasiri kwamba tumuombapo Mungu kutupa watu, atatupa.

Yesu anasema kama vile wazazi wema wasivyoweza kuwapatia watoto wao vitu vibaya, tunapomuomba kitu, hataweza kututega. Kwa hiyo omba kwa ajili ya watu sahihi kuja katika maisha yako kwa wakati sahihi. Na unapoomba, msikilize Roho Mtakatifu atakachokuamuru kufanya. Yawezekana mtu akaingia kazini kwako siku moja ambaye unaweza kumwomba mkale pamoja. Labda yaweza kuwa ni nafasi ya kumfahamu mtu unayetumika naye kanisani.

Lakini hapa kuna jaambo. Kutafuta matafiki inahitaji kuchukua hatua nje ya sehemu yako ya starehe na utambue kwamba wakati mwingine unaweza kukataliwa. Ili kupata sehemu halisi unayostahili katika maisha, lazima ujitolee. Lazima ujitose pasipo kujua jinsi itakavyokuwa na nani atakupokea au kukukubali. Kwa sababu Kukabiliana na hofu ya kukataliwa ni ufunguo wa kufahamiana.

Kwa hiyo, unapoona kwamba kuna mtu unatakiwa kumfikia, fanya hiyo! Huwezi jua kama utakuwa jibu la ombi lao kwenye jumuiya. 

Fikiria: Ni watu gani Mungu amewaweka katika maisha yako? Jinsi gani unaweza kuchukua hatua na kufanya urafiki nao?

Omba: Mungu, asante kwa kuwa baba mwema anayejali kila sehemu maisha yetu. leo, ninakuomba uwalete watu katika maisha yangu. Nisaidie ujasiri kushinda hofu ya kukataliwa na kupata marafiki wa kweli. Nipe ujasiri wa kumkaribisha mtu katika maisha yangu juma hili. Katika jina la Yesu. Amen. 

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Collective: Finding Life Together

Unapofikia umri wa miaka 18, unaanza kuona kwamba unahitaji kupanga maisha yako. Itakuwaje usipofanya hivyo? Itakuwa kama ulipofikiria utakuwa sipo ulipo sasa? Hauko peke yako. Hebu tuangalie swali kuu la maisha yetu pamoja katika mpango huu wa Biblia wa siku 7 kwa pamoja, mafunzo ya vijana kutoka Life. Church.

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/