Kwa pamoja: Kutafuta maisha pamojaMfano
Je, kila mtu ni mpweke kama nilivyo?
Taarifa inapatikana kwetu masaa 24 siku 7 siku hizi. Unaweza kutafuta kwenye google wakati wowote na sehemu yoyote. Unaweza pia kupata kwenye YouTube jinsi ya kuziba tairi, jinsi ya kufanya makisio, au jinsi ya kutengeneza chakula. Na wakati elimu hiyo inafaida, unaweza kupata elimu hiyo peke yako- kitu ambacho sicho tulichokusudiwa.
Mungu alituumba tuishi kwenye jumuiya. Hilo ndilo neno linalotumika mara nyingi kanisani ambalo kimsingi linamaanisha tunahitaji marafiki wazuri. Kwa nini? Kwa sababu kupata taarifa peke yako ni nadra sana kukubadilisha. Tunahitaji hekima, na hekima hukua vizuri kwenye jumuiya.
Hebu tuangalie mwanzo. Kitu cha kwanza Mungu alichosema ni " si vyema" mtu akawa peke yake. Tuliumbwa kuhitaji watu. Yesu alituonesha katika maisha yake na huduma yake duniani.
Yesu alichagua watu 12 wasio wakamilifu ili kuishi nao. Walikula pamoja, waliomba pamoja, na walihudumu pamoja. Kwa nini alifanya hivyo? Yesu hakuhitaji watu. Yesu anajitosheleza. Labda ilikuwa ni kutuonesha jinsi ya kupenda watunwasiokuwa wakamilifu kwa ajili ya kusudi lake kamilifu.
Yesu alituonesha inakuwaje kuwa na marafiki wazuri. Na alijua itamgharimu. Alijua Yuda atamsaliti. Kwa kweli, Petro wakati mwingine alizidi. Alijua Petro atamkana, lakini Yesu alimpenda siku zote.
Kuna somo tunaweza kujifunza kutokana na upendo wa jinsi hiyo. Mara nyingi tunaweza kuwa tunawatafuta marafiki wakamilifu na kukosa wale wenye uwezo mbele yetu. Tunapowapata watu, tunahitaji kuwapenda- mapungufu yao- kama Yesu anavyotupenda.
Faida nyingine ya jumuiya ni kwamba si kwamba Yesu alituonesha mfano tu lakini pia alituahidi yeye kuwa kati yetu. Yesu alisema kwamba wawili watatu wakusanyikapo kwa jina lake, Yupo kati kati yao. Hiyo ni sababu ya lazima kutumia muda wako na watu wengine.
Kwa hiyo kama unajaribu kufikiria mpango wa maisha yako bila kuzungukwa na watu, yawezekana isiwe kama ulivyotarajia. Tunahitaji watu ili tuweze kuyaishi makusudi yetu. Tunahitaji watu ili tujijue sisi ni nani. Tunahitaji watu kututia moyo, kututia nguvu, kuomba nasi, kutupa changamoto, na kutuinua tunapoanguka na kushindwa.
Tutaharibikiwa. Na haitakuwa na maana. Lakini tukichagua kuwa kama Yesu na kupenda kama Yesu- utatambua kwamba unaelekea katika njia bora kama tuliyosema siku ya kwanza.
Fikiria: Marafiki gani wa maana unawakosa kwa sababu unataka walio wakamilifu?
Omba: Yesu, nakushukuru kwa kutuonesha jinsi ya kuwa na jumuiya na kwa kuahidi kuwa pamoja nasi tunapokusanyika pamoja. Nisaidie nikutegemee zaidi na wengine uliowaweka maishani mwangu. Nisaidie kuwapenda kama wewe. Katika jina lako. Amen.
Kuhusu Mpango huu
Unapofikia umri wa miaka 18, unaanza kuona kwamba unahitaji kupanga maisha yako. Itakuwaje usipofanya hivyo? Itakuwa kama ulipofikiria utakuwa sipo ulipo sasa? Hauko peke yako. Hebu tuangalie swali kuu la maisha yetu pamoja katika mpango huu wa Biblia wa siku 7 kwa pamoja, mafunzo ya vijana kutoka Life. Church.
More