INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SITAMfano
MFANO WA MPANZI
"1 Siku iyo hiyo Yesu akatoka nje ya nyumba akaketi kando ya bahari.
2 Umati mkubwa mno wa watu ukakusanyika kumzunguka hata ikabidi aingie katika chombo na kuketi humo, nao watu wote wakawa wamesimama ukingoni mwa bahari."
3 Ndipo akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema:
“Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake.
4 Alipokuwa akipanda, baadhi zikaanguka kando ya njia, ndege wakaja na kuzila.
5 Nyingine zikaanguka sehemu yenye mawe, ambapo hapana udongo mwingi. Zikaota haraka kwa sababu udongo ulikuwa hauna kina.
6 Lakini jua lilipozidi, mimea hiyo ilinyauka na kukauka
kwa sababu mizizi yake haikuwa na kina.
7 Mbegu nyingine zilianguka katikati ya miiba, miiba hiyo ikakua ikazisonga.
8 Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri ambapo zilitoa mazao, nyingine mara mia moja, nyingine mara sitini na nyingine mara thelathini.
9 Yeye mwenye masikio ya kusikia na asikie.”
18 “Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi:
19 Mtu ye yote anaposikia neno la Ufalme, naye asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake, hii ndiyo ile mbegu iliyopandwa kando ya njia.
"20 Ile mbegu iliyopandwa kwenye sehemu yenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na mara hulipokea kwa furaha.
21 Lakini kwa kuwa hana mizizi yenye kina ndani yake, lile neno hukaa kwa muda mfupi. Inapotokea dhiki au mateso kwa ajili ya hilo neno, yeye mara huchukizwa."
22 Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno, lakini masumbufu ya dunia na ushawishi wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda.
23 Lakini ile mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu ambaye hulisikia neno na kulielewa. Naye hakika hutoa matunda, akizaa mara mia, au mara sitini, au mara thelathini ya mbegu iliyopandwa.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org