INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SITAMfano
YESU APONYA VIPOFU WAWILI NA BUBU
27 Yesu alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata, wakipiga kelele kwa nguvu na kusema,
“Mwana wa Daudi, tuhurumie!”
28 Alipoingia mle nyumbani wale vipofu wakamjia. Akawauliza,
“Mnaamini kwamba ninaweza kufanya jambo hili?”
Wakamjibu, “Ndiyo, Bwana.”
29 Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema,
“Iwe kwenu sawasawa na mnavyoamini.”
30-31 Macho yao yakafunguka. Yesu akawaonya vikali, akisema,
“Angalieni mtu ye yote asijue kuhusu jambo hili.”
31 Lakini wao wakaenda na kueneza habari zake katika eneo lile lote.
32 Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Yesu.
33 Yule pepo mchafu alipotolewa, yule mtu aliyekuwa bubu akaongea. Ule umati wa watu ukastaajabu na kusema, “Jambo kama hili kamwe halijapata kuonekana katika Israeli.”
34 Lakini Mafarisayo wakasema,
“Huyo anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa mkuu wa pepo wachafu.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org