Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMIMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI

SIKU 6 YA 7

  

YESU AINGIA YERUSALEMU KWA SHANGWE

1 Walipokuwa wanakaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika Mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili,akiwaambia,

“Ingieni katika kijiji kilichoko mbele yenu, nanyi mtakuta punda amefungwa na mwana-punda pamoja naye. Wafungueni na mniletee.

3 Kama mtu ye yote akiwasemesha lo lote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara moja.”

4 Haya yalitukia ili litimie lile lililonenwa na nabii, akisema:

5 “Mwambieni Binti Sayuni, ‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako, ni mnyenyekevu, naye amepanda punda,

juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’ 

6 Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama vile Yesu alivyokuwa amewaagiza.

7 Wakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda na Yesu akaketi juu yake.

8 Umati mkubwa wa watu wakatandika nguo zao barabarani na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti wakayatandika barabarani.

9 Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema,

“Hosana Mwana wa Daudi!”“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”“Hosana juu mbinguni!”

10 Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?”

11 Ule umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana

More

Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org