Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMIMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI

SIKU 4 YA 7

  

YESU AMPONYA MWOMBAJI KIPOFU

"35 Yesu alipokuwa anakaribia Yeriko, kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada.Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita, akauliza, “Kuna nini?” Wakamwambia,“Yesu wa Nazareti anapita.”

38 Akapaza sauti, akasema, “Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu!”

39 Wale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, unirehemu!”

40 Yesu akasimama, akawaamuru huyo mtu aletwe kwake. Alipokaribia, 

Yesu akamwuliza,

41 “Unataka nikufanyie nini?” Akajibu, “Bwana, nataka kuona.”

42 Yesu akamwambia, “Basi upate kuona, imani yako imekuponya.”

43 Akapata kuona saa ile ile, akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana

More

Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org