INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMIMfano
YESU ALAANI MTINI USIOZAA, YESU AWAFUKUZA WATU KUTOKA HEKALUNI NA WAULIZA KUHUSU MAMLAKA YA YESU
12 Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, Yesu alikuwa na njaa. Alipouona mtini kwa mbali, akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini. Yesu akauambia ule mti, Tangu leo mtu ye yote na asile kamwe matunda kutoka kwako.”
Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.
15 Walipofika Yerusalemu, Yesu akaingia Hekaluni akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wananunua na kuuza humo ndani.
"Akapindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa,wala hakumruhusu mtu ye yote kuchukua bidhaa kupitia ukumbi wa Hekalu.
17 Naye alipokuwa akiwafundisha, akasema, “Je, haikuandikwa kuwa:
“ ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote’? Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyang'anyi.’ ”
Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria wakapata habari hizi, nao wakaanza kutafuta njia ya kumwua, kwa kuwa walikuwa wakimwogopa, kwa sababu umati wote wa watu walikuwa wanashangazwa na mafundisho yake.
19 Ilipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake wakatoka nje ya mji.
20 Asubuhi yake, walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umenyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. Petro akakumbuka na kumwambia Yesu, “Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!”
22 Yesu akawajibu akawaambia, “Mwaminini Mungu.
23 Amin, amin nawaambia, mtu ye yote atakayeuambia mlima huu, ‘Ng'oka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
27 Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea Hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia. 28 Wakamwuliza,
“Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Naye ni nani aliyekupa mamlaka ya kufanya hayo?”
29 Yesu akawajibu, “Nitawauliza swali moja. Nijibuni, nami nitawaeleza ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.
30 Niambieni, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?”
31 Wakasemezana wao kwa wao, wakisema, “Kama tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’
32 Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ (Waliwaogopa watu, kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yohana alikuwa nabii kweli kweli.)
33 Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Hatujui.” Naye Yesu akawaambia,
“Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org