INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA TATUMfano
KUPAA KWA YESU
LUKE 24
44 Akawaambia, “Haya ndiyo yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Torati ya Mose, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”
45 Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko. Akawaambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu.
47 Toba na msamaha wa dhambi utatangazwa kupitia jina lake, kuanzia Yerusalemu.
48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.
49 “Tazama nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu, lakini kaeni humu Yerusalemu mpaka mtakapovikwa uwezo utokao juu.”
50 Akiisha kuwaongoza mpaka kwenye viunga vya Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki.
51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni.
ACTS 1
9 Baada ya kusema mambo haya, walipokuwa wanatazama, akachukuliwa juu mbinguni mbele ya macho yao na wingu likampokea wasimwone tena. Walipokuwa bado wakikaza macho yao kuelekea juu alipokuwa akienda zake Mbinguni, ghafula, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe wakasimama karibu nao, wakasema,
“Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama juu angani?
Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda Mbinguni, atarudi tena jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake Mbinguni.”
LUKE 24
52 Kisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu.
53 Nao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kumshukuru Gnpi-Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org