INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA TATUMfano
YESU KUWAONEKANIA WAFUNZI NA TOMASI
19 Ikawa jioni ya ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walipokuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi,
Yesu aliwatokea, akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi.”
20 Baada ya kusema haya, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi wake wakafurahi sana walipomwona Bwana. Yesu akawaambia tena,
“Amani iwe nanyi! Kama vile Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi.”
22 Naye alipokwisha kusema haya, akawavuvia, akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. Mkimwondolea mtu ye yote dhambi zake, zitaondolewa na ye yote mtakayemfungia dhambi zake, zitafungiwa.”
24 Lakini Tomasi, aliyeitwa Didimasi, yaani, Pacha, mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Yesu alipokuja. Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.”
Lakini yeye akawaambia, “Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini.”
26 Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomasi alikuwa pamoja nao. Ndipo Yesu akaja milango ikiwa imefungwa na kusimama katikati yao akasema, “Amani iwe nanyi.”
27 Kisha akamwambia Tomasi, “Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu.”
28 Tomasi akamwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu!”
29 Yesu akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.”
30 Yesu alifanya miujiza mingine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki.
31 Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kumshukuru Gnpi-Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org