INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA TATUMfano

YESU AMREJESHA PETRO
1 Baada ya haya Yesu akawatokea tena wanafunzi wake kando ya Bahari ya Tiberia. Yeye alijionyesha kwao hivi:
2 Simoni Petro, Tomasi aitwaye Didimasi, yaani Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja.
3 Simoni Petro akawaambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.” “Tutakwenda pamoja nawe.”
Nao wakamwambia, Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua, lakini usiku ule hawakupata cho chote.
4 Mara baada ya kupambazuka, Yesu akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Yesu. Yesu akawaambia, “Wanangu, je, mna samaki wo wote?”
Wakamjibu, “La.”
6 Akawaambia, “Shusheni nyavu upande wa kuume wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.”
"Wakashusha nyavu na tazama wakapata samaki wengi mno hata wakashindwa kuvutia zile nyavu zilizojaa samaki ndani ya mashua.
7 Yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro,
“Huyu ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia haya, akajifunga nguo yake kwa kuwa alikuwa uchi, naye akajitosa baharini.
8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliyojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa 200. Walipofika pwani, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake na mikate.10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi.”
11 Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu pwani. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa 153. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. “Njoni mpate kifungua kinywa.”
12 Yesu akawaambia, Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Kwa sababu walijua ya kuwa ni Bwana.
13 Yesu akaja, akachukua ule mkate, akawapa na vivyo hivyo akawagawia pia wale samaki. Hii ilikuwa mara ya tatu Yesu kuwatokea wanafunzi wake tangu afufuke kutoka kwa wafu.
15 Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?”
Yeye akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.”
Yesu akamwambia, “Lisha wana-kondoo wangu.”
16 Yesu akamwambia tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.”
Yesu akamwambia, “Chunga kondoo zangu.”
17 Kwa mara ya tatu Yesu akamwuliza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzunika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, “Unanipenda?”Akamjibu, “Bwana, wewe unajua yote, unajua ya kuwa ninakupenda.”
Yesu akamwambia, “Lisha kondoo zangu.
24 Huyu ndiye yule mwanafunzi anayeshuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.
25 Lakini kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya. Kama yote yangeliandikwa,
nadhani hata ulimwengu wote usingekuwa na nafasi ya kutosha kuweka vitabu vyote ambavyo vingeandikwa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kumshukuru Gnpi-Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org