Soma Biblia Kila Siku 6Mfano
Ikawa huko Ikonio wakingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi; na kwa vile walivyonena, kundi kubwa la Wayahudi na la Wayunani wakaamini (m.1). Maelezo: 1. Wayahudi hawakukaa katika nchi ya Israeli tu bali walikuwa wameenea katika nchi zote na miji yote mikubwa. 2. Kila mahali walipokaa walikuwa wamejenga sinagogi. Kazi yake ilikuwa kama jengo la kanisa kwetu. 3.Utaratibu wa Paulo kila mahali alipofika ni kwanza kuingia katika sinagogi ili kuhubiri Injili, maana Injili ni kwa Wayahudi kwanza: Injili ... ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia(Rum 1:16).4. "Wayuani" ni Mataifa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz